Welcome to our consulting company Consultio!
call4predictioncall4predictioncall4prediction
(Sat - Thursday)
Melbourne, Australia
call4predictioncall4predictioncall4prediction
0

Muongozo wa Kubeti Soka

Muongozo wa Kubeti Soka

Soka ni mchezo maarufu zaidi duniani, hivyo basi kuna idadi kubwa ya watu wanaojiita ‘wataalamu’ wa mchezo huo ambao wanafikiri wanajua kila kitu kuhusu kubeti kuhusu kubeti mpira.
Watu hao wanawaaminisha wakamaria wengi wanaochipukia kuwa wanaweza kubashiri kwa usahihi zaidi na mara nyingine wanawatoza pesa kupelekea upotevu wa pesa hizo.
Ukweli ni kwamba, ‘football betting’ sio rahisi kiasi hicho, lakini pia sio ngumu kiasi cha kutosha kwa wewe kuwaamini wengine na kuwapa pesa zako ili tu wabashiri kwa niaba yako. Hakuna anaejua kila kitu, hivyo na wao. Pia hakuna asiejua kila kitu, hivyo na wewe. Kubeti katika soka ina faida kwa wale wanaotumia muda wao kusoma na kuchambua kila taarifa muhimu kuhusu mechi husika.
Kama tungekua tunajadili kuhusu uchaguzi wa kampuni bora ya kubeti, wala kusingekuwa na haja ya kutumia nguvu na muda mwingi kwani jibu ni ‘Sokabet’ lakini hilo silo tunalojadili hapa.
Lengo la muongozo huu ni kuwapa mwanga wakamaria wote, wazoefu kwa wasio wazoefu kuhusu football betting.
Baadhi ya Masoko Muhimu katika Football Betting
Kwa kuanzia tutajadili kuhusu masoko muhimu na maarufu zaidi ya kuweka bashiri katika soka. Hata kama unafikiri tayari unaujuzi juu ya haya masoko ningekushauri usiache kusoma hapa kwani kujifunza hakuna mwisho.
Win-Draw-Win
Soko hili linafahamika pia kama 1 × 2, juna lake linajieleza. Kwa kutumia soko hili mkamaria anao uwezo wa kubashiri juu ya matokeo halisi ya mechi ndani ya dakika 90 (pamoja na zile za nyongeza).
Mkamaria anaweza kuchagua timu ya nyumbani ishinde, mechi iishe kwa sare au timu ya ugenini ishinde.
Win-draw-win ni soko maarufu zaidi katika ulimwengu wa kubeti, labda kwa sababu kuchagua tu timu gani itashinda ni rahisi kuliko masoko mengine kama handcaps na ‘totals’.
Double Chance
Ni soko linalomuwezesha mkamaria kuweka machagulio mawili ya matokeo katika matatu yanayopatikana, hii inaifanya kuwa na odds chache kulinganisha na win-draw-win.
Soko hili linamuwezesha mkamaria kuipa timu ya nyumbani ishinde au itoe suluhu, pia anaweza kuipa timu ya ugenini ishinde au itoe suluhu, pia anaweza kuweka uchaguzi wa timu yoyote ishinde, kwa uchaguzi huu wa mwisho (12) ili mkamaria ashinde bet yake ni lazima timu yoyote iondoke na ushindi, yani kusiwepo na sare.
Juu ya/Chini ya Magoli 2.5
Katika soko hili, mkamaria anaweka bashiri katika jumla ya idadi ya magoli yatakayopatikana katika mchezo husika. Kama mkamaria anafikiri mechi itaisha na jumla ya magoli 3 na kuendelea anaweza Over 2.5 (magoli kuanzia 3 na kuendelea), ila kama anafikiri mechi hiyo itaisha na magoli chini ya 3 anaweka under 2.5 (magoli 0, moja au mawili).
Soko hili ni rahisi kwa wale wakamaria ambao wanafikiri baada ya kufanya uchambuzi wa kina, kuwa mechi itakua na magoli mengi au machache lakini hawana uhakika wa kutosha juu ya timu gani itaibuka mahindi wa mechi.
Soko hili lina masoko mengine yanagohusiana kama vile Juu ya/Chini ya 0.5, 1.5, 3.5, 4.5 na 5.5, lakini Juu ya/Chini ya 2.5 ndilo soko maarufu zaidi katika kundi lake.
Correct Score
Hili linasemekana kuwa moja kati ya masoko magumu zaidi kubashiri kwa usahihi, ‘correct score’ ni soko linalopendwa na wakamaria wachache. Soko hili linawawezesha wakamaria kubashiri matokeo halisi ya mchezo. Mtu anaweza kubashiri kuwa mechi itaisha kwa matokeo ya 0-0, 1-0, 1-1, 2-0 au 2-1 na kadhalika, mechi ikiisha kwa matokeo hayo bet inakua imeshinda.
Ugumu wa kubashiri matokeo halisi ya mchezo umefanya soko hilo kiwa na odds nyingi kulinganisha na masoko mengine. Lakini ni muhimu kwa mkamaria kuweka akilini kuwa ukubwa au udpgo wa odds haitakiwi kuwa kigezo cha kuchagua soko fulani.
Handicap
Soko hili lina lengo la kuweka uwanja sawa wa kuchezea kwa timu hasa mechi ikiwa inahusisha timu inayoonekana kuwa bora sana ikiwa inacheza dhidi ya ile inayoonekana kiwa dhaifu sana.
Kwa kawaida, timu imara itapewa handicap ya -1.5 kumaanisha kwamba mechi itaanza timu hiyo ikiwa imefungwa magoli mawili (hesabu hiyo ni katika betting tu na haihathiri uhalisia wa mechi husika), hii ji sawa na kusema ile timu dhaifu itaanza ikiwa na magoli mawili mkononi.
Kwa urahisi tuseme unapoweka bashiri ya handicap ya -1.5 kwa timu ya nyumbani labda, ili bet yako ishinde itatakiwa timu hiyo ishinde kwa ushindi wa magoli mawili au zaidi. Ila kama ukiweka bashiri ya +1.5, bashiri yako itakuwa ‘won’ ikiwa mechi itaisha kwa timu yako kushinda ushindi wowote, sare yoyote, au kupoteza kwa goli moja.
Half-Time/Full-Time (HT/FT)
Soko hili linamuwezesha mkamaria kubashiri matokeo ya mchezo kwa kipindi cha kwanza au matokeo ya mwisho ya mchezo husika. Katika soko hili mkamaria anaweza kubashiri mshindi wa kipindi cha kwanza (au hata kama ni sare) kisha mshindi wa mechi nzima (hata kama ni sare).
Unaweza kubashiri kuwa mechi mapumziko ikiwa sare, lakini timu ya nyumbani kushinda mwisho wa mchezo ( au vyovyote unavyoona itakuwa).
Kwa urahisi zaidi tuseme, HT/FT ni soko linalomuwezesha mkamaria kubashiri matokeo ya kipindi cha kwanza na pia matokeo ya mwisho ya mchezo.
Kwa mfano ukiweka bet kwa timu ya nyumbani kushinda kipindi cha kwanza na matokeo ya jumla (1/1) na matokeo yakawa 1-0 mapumziko, na pia mechi ikaisha hivyo hivyo 1-0 ubashiri huo unakua umeshinda.
Kuna Masoko Mengine Pia
Kuna mamia kama sio maelfu ya masoko katika uwanja wa football betting.
Uwepo wa masoko mengi ya kubashiri ni faida na hasara kwa pamoja. Ni faida kwa sababu inakuwezesha kuchagua soko unalolipenda au unaloona linafaa zaidi kwa mechi husika, lakini ni hasara kwa sababu inaweza kumchanganya mkamaria akajikuta anaacha soko zuri na kupotoshwa na jingine baya.
Kitu muhimu ni kujifunza zaidi kuhusu footbll betting, kufanya uchambuzi wa kina kwa mechi husika kwa kuangalia vitu muhimu kama ‘head to head performance’ ya timu husika, ‘performance’ ya timu hizo kwa mechi kadhaa zilizopita, vikosi vya timu husika na kadhalika lakini pia kuwa na nidhamu na sio kuchagua tu soko fulani kwakua lina odds chache au nyingi.

Namna ya Kupata Faida Katika Fotball Betting
Kitu cha kwanza na muhimu zaidi kukifahamu katika football betting ni kuwa, ‘hakuna kitu cha uhakika’ kwenye soka, lolote linaweza kutokea. Na pia hatupo hapa kikwambia kuwa baada ya kusoma makala hii utashinda kila bet utakayoweka, lengo ni kupata faida katika betting.
Unaweza kusoma hapa, ukafanya uchambuzi kadri uwezavyo kuhusu mechi husika, lakini bado lolote linaweza kutokea katika soka.
Binafsi naoma inplay bettings ni rahisi zaidi kwa kuwa inampa mkamaria uwanja wa kubet akiwa ameusoma mchezo husika na kujua lipi ni chaguo sahihi zaidi.
Lakini pia, wakamaria wasio wazoefu wanashauriwa kuweka bashiri kwenye masoko rahisi kama win-draw-win, totals na Double Chance huku wakijifunza zaidi.
Wakamaria wote, wazoefu kwa wasio wazoefu wanashauriwa kuweka bashiri zao kwenye ligi za soka ambazo wamezizoea au wanazifahamu zaidi kuliko zile wasizokua na uzoefu nazo.

Leave A Comment

No products in the cart.

Subscribe to our newsletter

Sign up to receive latest news, updates, promotions, and special offers delivered directly to your inbox.
No, thanks
X